HIKI hapa kikosi kazi cha Azam FC ambacho kipo Libya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Akhdar ya Libya.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 8,2022.
Ali Ahmada, Ahmed Salula, Zuber Foba ni kwa upande wa makipa. Mabeki ni Lusajo Mwaikenda, Nathan Chilambo, Bruce Kangwa, Agrey Moris, Malickou Ndoye, Daniel Amoah, Edward Manyama, Abdallah Kheri na Pascal Msindo.
Upande wa viungo ni James Akaminko, Cleophance Mkandala,Isah Ndala, Abdul Suleiman, ‘Sopu’, Kipre Junior, Yahya Zayd, Idd Nado, Tape Edinho, Ayoub Lyanga, Tepsie Evance, Sospeter Bajana.
Ni washambuliaji wawili wapo ndani ya kikosi kazi ambao ni Idris Mbombo na Prince Dube na mastaa hawa wote kwenye ligi wametupia bao mojamoja.