ZINCHENKO, ODEGAARD KUIWAHI DABI

MASTAA wawili wa Arsenal, Oleksandr Zinchenko na Martin Odegaard, imeelezwa kuwa watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Dabi ya London Kaskazini dhidi ya Tottenham, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi ijayo.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa shauku kubwa itapigwa kwenye Uwanja wa Emirates huku ikizikutanisha timu hizo zilizopo ndani ya Top 3 kwenye Premier kwa sasa.

Zinchenko aliukosa ushindi wa 3-0 dhidi ya Brentford Jumapili iliyopita kutokana na majeraha na kumfanya akose jumla michezo mitatu ya timu hiyo kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kigimbi cha mguu huku nahodha Odegaard naye akikosekana kutokana na kutokuwa fiti.

Kwa mujibu wa Metro, wote hao wanatarajiwa kurejea uwanjani katika mchezo ujao dhidi ya wapinzani wao kisha kete ijayo inatarajiwa kuwa dhidi ya Liverpool.