Home Sports U 23 YATOSHANA NGUVU NA SUDAN KUSINI AZAM COMPLEX

U 23 YATOSHANA NGUVU NA SUDAN KUSINI AZAM COMPLEX

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 leo Septemba 23 kimelazimisha suluhu dhidi ya Timu ya Taifa ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON.

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo wageni Sudan Kusini walicheza kwa umakini wakitumia mbinu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

U 23 ilianza kwa kasi kuliandama lango la Sudan Kusini lakini umakini ulikosekana ndani ya dakika 15 za mwanzo kuweza kupata bao la kuongoza.

Nahodha wa U 23, Kelvin John amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo lakini imeshindikana hivyo benchi la ufundi litaona namna ya kuboresha.

Kocha Mkuu wa U 23, Hemed Morocco amesema kuwa mapungufu ambayo wameyaona watayafanyia kazi kwenye mechi ya marudio.

“Wachezaji walicheza kwa kujitoa lakini muunganiko na umakini kwenye kumalizia nafasi ulifanya tukashindwa kupata matokeo, makosa ambayo tumefanya tutafanyia kazi na mchezo ujao tuna imani tutapa matokeo,”.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa nchini Rwanda hivi karibuni.

Previous articleMAYELE ATOA KAULI YA KIMATAIFA
Next articleNABI ATAKA KROSI, KONA BAO, MGUNDA ATENGA DAKIKA 180