ANAZIDI kuimarika akiwa langoni, Aboutwalib Mshery na alipewa dakika 90 mbele ya Zalan FC mchezo wa kwanza na ule wa pili alitumia dakika 45.
Sababu ya kupewa nafasi kikosi cha kwanza ni kutokana na maumivu ambayo alikuwa nayo kipa namba moja, Diarra Djigui hivyo kazi ikawa kwake kutimiza majukumu ya timu.
Kutinga hatua ya awali bila kuokota bao kwenye nyavu ni jambo kubwa na rekodi ya kujivunia kwa kila mchezaji.
Ushindi wa jumla ya mabao 9-0 ni deni kwa wachezaji kuonyesha kwamba hawakubahatisha bali ni uwezo waliutumia na kujituma bila kuogopa.
Tumeona, Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amebainisha kuwa kuna makosa kwenye matumizi ya nafasi zinazotengenezwa ndani ya uwanja.
“Tunatengeneza nafasi nyingi lakini imekuwa ngumu kuzitumia zote, kuna kazi ambayo tunapaswa kuifanya kwa mechi zijazo ili kuwa imara zaidi,” .