BILA KUFUNGWA KIMATAIFA SIMBA KAZI HAIJAISHA

DAKIKA 180 kimataifa dhidi ya Nyassa Big Bullets lango la Simba lilikuwa salama chini ya kiongozi Aishi Manula aliyekuwa langoni.

Huyu ni kipa namba moja ambaye anazidi kuwa imara kila anapokaa langoni na huwa anafanya makosa ambayo yanapelekea kufungwa.

Kufungwa haina maana kwamba hayupo imara hapana ni matokeo ambayo yanatokea uwanjani na wakati unakuja anafanyia kazi makosa hayo kwa kushirikiana na wachezaji wengine.

Kwenye safu ya ulinzi wapo wachezaji ambao anashirikiana nao kuweka ngome ya Simba imara.

Ni Henock Inonga huyu alikuwa msimamizi wa masuala ya ulinzi kwa upande wa mabeki akishirikiana na Israel Mwenda pamoja na Mohamed Hussein.

Bado kazi haijaisha kimataifa, hatua inayokuja ni ngumu kwa wawakilishi hawa wa Tanzania kufanya kweli na muhimu kufanyia kazi makosa yao.

Upande wa ushambuliaji huku ni tatizo pia hasa kwa kuwa na namba ndogo ya kutumia nafasi ambazo zinatengenezwa kimataifa.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amebainisha kuwa matatizo kwenye mpira lazima yatokee ili yafanyiwe kazi.

“Makosa yapo na hayo tunayafanyia kazi kwa ajili ya kuwa imara kwa mechi zetu zijazo na tunaamini kwamba tutarejea tukiwa imara,”.

Mabao manne bila kufungwa ni hatua inayohitaji kuendelea ili kufika mbali zaidi ya hapa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari wapinzani wa Simba wameshajulikana ambao ni de Agosto  mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 7.

Imeandikwa na Dizo Click