HESABU ZA YANGA KIMATAIFA ZINAENDELEA KWA MTINDO HUU

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameanza kuwafuatilia wapinzani wake kimataifa katika hatua ya awali Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 7 na 9 Uwanja wa Mkapa.

Yanga imetinga hatua hiyo kwa jumla ya ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Zalan FC katika mechi mbili ambazo wamecheza.

Ni Al Hilal ya Sudan itamenyana na Yanga katika hatua inayofuata na iliwaengua wapinzani wao St George ya Ethiopia.

Kutokana na hali hiyo tayari benchi la ufundi lilifanikiwa kuutazama mchezo huo kwa umakini ili kuweza kupata mbinu za kuwakabili wapinzani wao.

Habari zinaeleza kuwa benchi la ufundi liliufuatilia mchezo huo kwa umakini ili kupata mbinu mpya za kuwakabili wapinzani wao.

“Mchezo wa kimataifa wa Al Hilal na St George benchi la ufundi liliutazama na hapo kuna picha imepatikana kuelekea mechi zetu za kimataifa na kikubwa ni kupata matokeo chanya,” ilieleza taarifa hiyo.

Nabi hivi karibuni alisema kuwa kila mechi huwa anafuatilia hasa ambazo zinawahusu wapinzani wao.

“Huwa ninapata muda wa kutazama mechi za wengine na hii inanipa kitu kwa ajili ya mechi zetu zijazo,”.