Home Sports MATOKEO MABAYA YANALETA MTIKISIKO

MATOKEO MABAYA YANALETA MTIKISIKO

MTIKISIKO unapatikana kila baada ya matokeo mabaya kwenye mioyo ya Watanzania baada ya matokeo mabovu huwa ni mkubwa.

Hili linatokana na namna ambavyo kila mmoja anapenda kuona mafanikio kwa wachezaji wa ndani wanaocheza timu ya taifa.

Haiajalishi ni Timu ya Taifa ya Wanawake, Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ama timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kikubwa ni matokeo.

Kwa sasa kwa upande wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni wapo kwenye maandalizi ya COSAFA ambayo ni mashindano makubwa na muhimu.

Septemba 25-Oktoba Mosi 2022 yanatarajiwa kufanyika haya mashindano huko Durban, Afrika Kusini.

Kikubwa kwa muda huu wa maandalizi mipango muhimu ya ushindi inahitajika na wachezaji kujituma bila kuogopa kwenye msako wa matokeo.

Ukitazama mechi za hivi karibuni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni haikuwa na mwendo mzuri kutokana na kushindwa kupata matoke chanya.

Hata timu ya Taifa ya Wanaume nayo ilikwama kufanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni hapo unaoa kuwa mtikisiko ni mkubwa kwenye mioyo ya Watanzania.

Weka kando hayo kazi inayofuata kwa kila mchezaji ambaye ameitwa kikosi cha timu ya taifa jambo lake ni moja afanye kazi mwanzo mwisho.

Tunawaamini wachezaji mnaweza ila kuaminiwa kwenu kulete majibu ya kweli kwa kila mtakachokifanya uwanjani.

Kila la kheri wachezaji wote mlioitwa kwenye timu na Watanzania wanapenda furaha ambayo inatokana na matokeo mazuri.

Taifa Stars tayari imeshakwea pipa kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki ambazo zipo ni dhidi ya Uganda na Libya, kinachohitajika ni maandalizi.

Previous articleSAUTI: WAJUE WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA
Next articleHESABU ZA YANGA KIMATAIFA ZINAENDELEA KWA MTINDO HUU