Home Sports KMC YASHINDA KWA MARA YA KWANZA NDANI YA LIGI

KMC YASHINDA KWA MARA YA KWANZA NDANI YA LIGI

KMC leo imepata ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Uhuru kusoma KMC 2-1 Ihefu FC.

Ni mshambuliaji mzawa, Matheo Anthony alipachika bao la mapema dakika ya 3 huku Raphael Daud dakika ya 34 aliweka usawa kwa Ihefu na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.

Kipindi cha pili KMC walianza kwa kasi kuliandama lango la Ihefu na walipata bao la ushindi dakika ya 77 kupitia kwa Nzigamasabo Styve.

KMC inafikisha pointi tano ikiwa nafasi ya 8 huku Ihefu ambayo ipo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi imegotea nafasi ya 16 ikiwa haijakusanya pointi.

Kwa msimu wa 2022/23 KMC imepata ushindi wake kwa mara ya kwanza huku Ihefu ikiwa bado haijapata kushinda.

Previous articleVIDEO:JEMBE AWACHAMBUA WAPINZANI WAO KIMATAIFA
Next articleSAUTI:AL HILAL YAMUIBUA SENZO YANGA