SIMBA HESABU ZAO NI KWA BIG BULLETS

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa wanatambua mchezo wao ujao dhidi ya Big Bullets utakuwa mgumu hivyo wanajipanga kupata matokeo.

Mgunda ana kibarua cha kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo ujao wa kimataifa ambao ni wa awali baada ya ule wa kwanza kushinda.

 Mchezo huo dhidi ya Big Bullets unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 18, saa 1:00 usiku.

Katika mchezo wa awali uliochezwa, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 hivyo wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na faida ya mabao mawili.

Mgunda amesema:”Kumaliza kazi ya kwanza inatupa hatua nyingine kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa pili ambao utakuwa mgumu.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu, ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa ambayo tuliyaona kwenye mchezo uliopita,” .

Ni mabao ya John Bocco na Moses Phiri yaliwapa ushindi Simba wakiwa ugenini kimataifa.