UWANJA wa Zimbru kwenye mchezo wa Europa kwa kundi E ni mabao mawili Sheriff walishuhudia yakizama nyavuni huku watupiaji wakiwa ni Jadon Sancho dakika ya 17 na Cristiano Ronaldo dakika ya 39.
Mabao ya nyota hao yaliwapa furaha mashabiki wa Manchester United ambao walikuwa wakihitaji kuona timu inashinda.
Bao la Ronaldo lilipachikwa kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya wazidi kuipa ugumu Sheriff kwenye kupindua meza katika mchezo huo.
Ni mashuti 11 walipiga Sheriff huku mawili yakilenga lango na United wao walipiga mashuti 8 huku manne yakilenga lango kwenye mchezo huo.
Ushindi huo unaifanya United kufikisha pointi tatu ikiwa nafasi ya pili huku Sherif ikiwa nafasi ya tatu na zote zina pointi tatu kwenye msimamo.