Home Sports NYOTA AZAM FC WAPEWA KAZI NGUMU

NYOTA AZAM FC WAPEWA KAZI NGUMU

MASTAA wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Denis Lavagne raia wa Ufaransa ambaye amepewa dili la mwaka mmoja kuiona timu hiyo wakiongozwa na mshambuliaji Prince Dube wamepewa kazi ngumu kufunga kila nafasi.

Azam FC baada ya kucheza mechi tatu, safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao matano na kinara ni kiungo Tepsi Evance mwenye mabao mawili na pasi moja ya bao huku Prince Dube yeye akiwa ametupia bao moja.

 Kali Ongala, kocha wa washambuliaji wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wote ikiwa ni pamoja na Dube, Sopu, Evance wanakazi ya kutumia nafasi wanazopata kufunga.

“Unajua kuna kitu ambacho kipo hasa kwa washambuliaji ambao ninawafundisha pamoja na wachezaji wote, hawa jukumu lao ni kufunga kwenye nafasi ambazo wanazipata lakini haiwezi kuwa hivyo haraka inahitaji muda.

“Washambuliaji hawa wanapewa mbinu taratibu wanazielewa na kwenye utendaji inaonekana hasa kwa pale ambapo wanatengeneza nafasi kinachobaki ni kumalizia kwa kufunga hilo linakuja kwa mechi zetu zijazo nina amini watafunga,” amesema Ongala.

Azam FC leo Septemba 13 ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Mbeya City yenye pointi 4 baada ya kucheza mechi tatu.

Previous articleMTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA
Next articleJUMA MGUNDA ALIANZA NA MAMBO HAYA SIMBA