MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema wanahitaji kupata ushind kwenye mechi zote ambazo watacheza ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Yanga.

Mtibwa Sugar imeanza msimu kwa mwendo wake ikiwa imecheza mechi tatu, ushindi ni kwenye mechi mbili ina sare moja pointi zake kibindoni ni 7.

Kifaru amesema kuwa wanatambua wana kazi ngumu ya kusaka ushindi kwenye mechi zao hilo linafanyiwa kazi.

“Kwetu sisi kila mchezo ni muhimu kushinda na tunatambua kwamba Yanga ni timu nzuri ina wachezaji wazuri ila nasi tupo vizuri tunahitaji pointi tatu kwenye kila mchezo.

“Wachezaji wanastahili pongezi hasa kwa kazi ambayo wanaifanya na benchi la ufundi nalo linafanya kazi kubwa, tuna amini kwamba tutawapa kile ambacho wanahitaji ambacho ni ushindi,” amesema Kifaru.

Mtibwa inakutana na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 40 za ligi bila kupoteza ndani ya dakika 3,600.

Septemba 13,2022 unatarajiwa kuchezwa mchezo huo wa ligi, Uwanja wa Mkapa.

Mtibwa Sugar mchezo wake wa mwisho kwenye ligi ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Ihefu inakutana na Yanga iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.