Home Sports JUMA MGUNDA ALIANZA NA MAMBO HAYA SIMBA

JUMA MGUNDA ALIANZA NA MAMBO HAYA SIMBA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ameanza kazi yake na kuanza na rekodi 7 akiwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Big Bullets uliochezwa Uwanja wa Bingu.

Mgunda ni kocha wa muda akichukua mikoba ya Zoran Maki aliyeiongoza Simba kwenye mechi mbili za ligi na rekodi zake zipo namna hii:-

Wazawa na wageni kukiwasha

Mgunda alishuhudia wachezaji wake wote wakionyesha ubora wao kwa kutimiza majukumu kwa kushirikiana kwenye idara ikiwa ni ile ya ushambuliaji na ufungaji.

Bao la kwanza lilifungwa dakika 28 ni mgeni, Moses Phiri kwa mtindo wa kubinuka alipachikaba bao hilo yeye ni raia wa Zambia aliibuka Simba akitokea Zanaco alitumia pasi ya mzawa Kibu Dennis aliyetoa kwa pigo la kichwa

Bao la pili lilifungwa na mzawa, John Bocco ambaye ni nahodha alitumia pasi ya Clatous Chama raia wa Zambia ilikuwa dakika ya 83.

Kwa upande wa safu ya ulinzi Henock Inonga raia wa dr Congo alikuwa kiongozi na aliweza kuokoa hatari dakika ya 10 huku Israel Mwenda ambaye ni mzawa naye alionyesha uwezo wake kwa kuwa kwenye utulivu katika mechi hiyo ngumu.

Super Sub

Mgunda alishuhudia Bocco akiwa ni super sub kwa kuwa aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Phiri. Bocco alitumia dakika 8 kufunga bao lake la kwana kimataifa msimu wa 2022/23.

Ushindi wa ugenini

Ni ushindi wa kwanza Mgunda anaupata ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ameanza ugenini kimataifa dhidi ya Big Bullets kwenye mchezo wa kimataifa akiwa ni mzawa wa kwanza kuiongoza Simba kwenye mechi za kimataifa kwa msimu wa 2022/23.

Clean Sheet

Air Manula, kipa namba moja wa Simba alianza kazi yake kwa kufanikiwa kuzuia wapinzani wao Big Bullets kumtungua na miongoni mwa mastaa waliokuwa wasumbufu alikuwa ni Chimwemwe Abdalah.

Hakuna kadi

Kiungo wa kazi ngumu ndani ya Simba, Sadio Kanoute aliyeyusha dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Erasto Nyoni, licha ya kutembeza mikato ya kimyakimya hakuonyeshwa kadi ya njano.

Mgunda anashuhudia mchezo wa kwanza timu hiyo inayeyusha dakika 90 bila kuonyeshwa kadi yoyote ile ya njano ama nyekundu.

Pasi zilitembea

Simba ingekuwa makini ingepata ushindi wa mabao zaidi ya mawili hasa kipindi cha kwanza walicheza kwa umakini mkubwa na pasi zilitembea.

Phiri alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 2, Pape Sakho alikosa nafasi tatu za kufunga dakika ya 7,33 na 48 na Sadio Kanoute naye alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 8.

Utulivu wakutosha

Licha ya kipindi cha pili Big Bullets kuongeza presha bado Mgunda aliweza kuwatuliza presha wachezaji wake na kuwafanya wacheze kwa utulivu.

Bao la Bocco lilionyesha hali hiyo iliyotengenezwa na Chama akiwa ndani ya 18 akionekana hana haraka na mwisho akatoa pasi iliyoleta bao.

Kuhusu ushindi huo Mgunda alisema: “Ni mpango kazi ambao ulipangwa na ukatumika uwanjani, pongezi kwa wachezaji makosa tunakwenda kufanyia kazi,” amesema.

Mchezo huo ulichezwa Septemba 10,2022 na miongoni mwa mastaa walioipa hongera Simba kwa ushindi huo ni pamoja na nyota wa zamani wa kikosi hicho Sharaf Eldin Shiboub.

Previous articleNYOTA AZAM FC WAPEWA KAZI NGUMU
Next articleKIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOINGIA KAMBINI KUIKABLI LIBYA