HIVI karibuni, staa wa Manchester City, Erling Haaland akiwa anakatiza mitaa ya Jiji la Manchester, shabiki mmoja wa Manchester United alisikika akimwambia ‘njoo United msimu ujao’.
Shabiki huyo alikuwa akimfuata Haaland huku akimpigia kelele za kumtaka ahamie United.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo aliwahi kutajwa kuingia kwenye hesabu za United wakati anatoka RB Salzburg akasajiliwa na Dortmund Januari 2022 kisha msimu huu ametua ndani ya City.
Nyota huyo amefunga mabao 10 ndani ya Ligi Kuu England ikiwa ni msimu wake wa kwanza na kwenye mabao hayo ana ha trick mbili.
“Haaland umekuja sehemu ambayo sio sahihi ya Manchester,” alisikika shabiki huyo akimwambia Haaland ambaye alimjibu: “Hapana ninaipenda City,” . Shabiki huyo aliendelea kusema: “Njoo kwetu basi msimu ujao,” .
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)