WAWAKILISHI WA TANZANIA KIMATAIFA MUHIMU KUJITOA

    WAWAKILISHI wa kimataifa leo wanatarajiwa kutupa ket zao kwenye mechi za awali kusaka ushindi ndani ya dakika 90 za awali kabla ya nyingine tena.

    Yanga wao watakuwa ugenini wakicheza na Zalan FC ya Sudan Uwanja wa Mkapa, Simba itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Big Bullets na KMKM wao watakuwa ugenini dhidi ya Al Ahly Tripol.

    Geita Gold watakuwa ugenini kwenye mchezo dhidi ya Hilal Al Sahil huku Azam FC wao wakisubiri mshindi wa jumla mchezo kati ya Al Akhdar ya Libya na Al Ahly ya Khartoum ya nchini Sudan.

    Al Hilal Wau ya Sudan wao watacheza na Kipanga FC hii ni ya Visiwani Zanzibar na hawa ni wawakilish wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.

    Haitakuwa kazi nyepesi kwenye kusaka ushindi hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo na kusonga mbele.

    Ambacho kinatakiwa kwa sasa wachezaji kujua kwamba ili kupata matokeo chanya ni lazima mikakati iliyopangwa na benchi la ufundi pamoja na kujitoa kwao ni muhimu.

    Vipaji vipo na uwezo upo ila usipotumika kwa akili kwenye mechi hizi za kimataifa basi maumivu yatakuwa juu yao na taifa kiujumla.

    Kila kitu kinawezekana ikiwa wachezaji wataamua na wajituma kutumia nafasi ambazo wanazitengeneza hata ikiwa ni tatu zote zikitumika ipasavyo zitawapa matokeo.

    Watanzania wanapenda kuona matokeo chanya na ili matokeo hayo yapatikane muhimu kila mmoja kutimiza wajibu wake.

    Ni moja ya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi inawezekana kwa kila mmoja kujituma na kufanya kazi kubwa kusaka ushindi.

    Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye mechi za kimataifa hii ni kubwa kwenye kusaka ushindi ili kuongeza nguvu kwa mechi zijazo.

    Previous articleSINGIDA BIG STARS KUTUMIA MBINU ZA RWANDA KWENYE LIGI
    Next articleJESHI LA YANGA DHIDI YA ZALAN FC KIMATAIFA