Home Sports TANZIA:DAKTARI SIMBA ATANGULIA MBELE ZA HAKI

TANZIA:DAKTARI SIMBA ATANGULIA MBELE ZA HAKI

TAARIFA iliyotolewa leo Septemba 2,2022 na Klabu ya Simba ni kuhusu kutangulia mbele za haki kwa daktari wa timu hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii: “Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu yetu ya wanaume (Senior Team) ambaye kwa sasa alikuwa daktari wa timu ya vijana (Youth Team).

 “Dkt. Yassin Gembe kifo hicho kimetokea leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,”.

Baada ya ujumbe huo familia ya mpira imeandika ujumbe wa kuguswa na taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na nyota wa zamani wa Simba, Hamisi Kiza, ‘Diego’ ambaye amesema:”Polse sana familia ya dokta, ulikuwa mtu mzuri sana, pumzika kwa amani.

Pumzika kwa amani.

Previous articleMUUZA DUKA ASEPA NA KITITA CHA 113,789,620 KUTOKA M-BET
Next articleVIDEO:KMC WATAJA SABABU ZA KUWATEMA MASTAA WAO, YAWATAJA YANGA