Home Sports TATU ZA KIMATAIFA SIMBA KUCHEZA, KUIBUKIA SUDAN

TATU ZA KIMATAIFA SIMBA KUCHEZA, KUIBUKIA SUDAN

KIKOSI cha Simba kitakuwa nchini Sudan kwa ajili michezo ya kimataifa ya kirafiki wakiwa wamealikwa kwenye michuano midogo iliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal.

Mechi tatu za kimataifa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu itacheza wakati huu ligi ikiwa imesisimama kwa ajili ya mashindano ya CHAN, Zoran Maki akisaidiana na msaidizi mzawa Seleman Matola ni miongoni mwa waliopo kwenye msafara utakaokuwa Sudan.

Ni dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Agosti 28, kisha watacheza dhidi ya Al Hilal ambao ni wenyeji na wanatarajia kucheza na AS Arta Solar ya Djibout Septemba 3, Uwanja wa Mkapa.

Maki amesema kuwa ni jambo kubwa wao kupata mechi za kimataifa na itawafanya waweze kuwa imara zaidi na kurekebisha makosa yao.

“Mechi ambazo tumezipata za kirafiki ni muhimu kwetu na tunaamini kwamba zitatupa kitu kingine kizuri ambacho tunakihitaji.

“Ukweli ni kwamba bado tunahitaji kuwa imara kwa ajili ya mechi zetu za kwenye ligi pamoja na mashindano ya kimataifa,” amesema.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi mbili ikiwa imeshinda zote mbele ya Geita Gold na Kagera Sugar.

Previous articleROCK ā€˜Nā€™ ROLL NA KUSHINDA OFA NA MIZUNGUKO YA BURE NA SLOTI NA FOREST ROCK
Next articleVIDEO:PACHA WA MAYELE AFUNGUKIA KUFUATWA NA VIONGOZI SIMBA