Home Uncategorized AZIZ KI,OKRA WAPEWA KAZI MAALUMU KWENYE DABI

AZIZ KI,OKRA WAPEWA KAZI MAALUMU KWENYE DABI

MASTAA wawili wapya kwenye timu zao ambazo zinatarajiwa kukutana leo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Azizi KI na Augustino Okra.

Leo Aziz KI ambaye ni ingizo jipya ambaye alijiunga na Yanga akitokea Klabu ya ASEC Mimosas atakutana na Okra ambaye alijiunga na Simba akitokea Klabu ya Bechem United ya Ghana.

Ni kazi ya kupiga mipira iliyokufa ambayo itakuwa itatokea kwenye mechi za leo kwa kuwa waliweza kufanya hivyo kwenye mechi za kimataifa za kirafiki.

Kwenye Wiki ya Mwananchi,wakati Yanga ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Vipers,Nasreddine Nabi aliweza kumshuhudia kijana wake Azizi KI akipiga jumla ya faulo mbili kwenye mchezo huo na Okra yeye aliweza kupiga faulo pia kwenye mchezo dhidi ya St George.

Mbali na hao kwa Yanga wanaye nyota Bernard Morrison ambaye ni mpigaji wa faulo na Simba yupo pia Nelson Okwa ambaye naye alikuwa na kazi ya kupiga mapigo huru.

Previous articleAZAMKA KUNOGESHWA NA RAYVANNY
Next articleNABI:TUNAHITAJI UTULIVU KUSHINDA