Home Sports AZAMKA INAWALETA ZESCO KESHO AGOSTI 14

AZAMKA INAWALETA ZESCO KESHO AGOSTI 14

KESHO Agosti 14 kikosi cha Azam FC kitashuka Uwanja wa Azam Compex ikiwa ni mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo ni kuhitimisha kilele cha Tamasha la AZAMKA ambalo ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wapya.

Kiingilio kwenye mchezo huo kwenye jukwaa la mzunguko ni 5,000 tu hivyo mashabiki wa Azam FC watakuwa na kazi ya kuweza kuona burudani hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua kwamba kazi yao itakuwa ni kwa mashabiki ambao wao watakuwa waratibu wa tamasha hilo.

Kwenye kilele cha tamasha kubwa la AZAMKA Klabu ya Azam FC itamenyana na Zesco United kutoka Zambia.

“Ni kwa ajili ya mashabiki na tuna amini kwamba watafurahia hili kwa kuwa tunairejesha timu na kuwapa furaha ili kurejesha morali ndio maana tunasema AZAMKA,” amesema Thabit.

Previous articleFT:YANGA 2-1 SIMBA UWANJA WA MKAPA
Next articleSAUTI:FISTON MAYELE YUPOYUPO SANA,ISHU YA KAIZER CHIEFS IPO HIVI