Home Sports YANGA YATAMBA KUKOMBA KILA KITU

YANGA YATAMBA KUKOMBA KILA KITU

NDANI ya Yanga kwa sasa ni raha na vicheko tu kutokana na fedha ambazo zinaendelea kuingia kwenye timu hiyo kupitia wadhamini ambapo mabosi wa timu hiyo mapema tu wametamba wanataka kubeba mataji yote kama msimu uliopita.

Mabosi hao wameongeza kuwa wanataka kubeba mataji yao yote waliyotwaa msimu uliopita ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports ikiwa ni mkakati wao wa kutawala soka la Tanzania.

Kauli hiyo ya kibabe inakuja baada ya timu hiyo wiki hii kusaini mkataba wa udhamini na Kampuni ya SportPesa wa bilioni 12.3 huku wakiwa na uhakika wa kuingiza zaidi ya bilioni moja kwa mwezi ukiunganisha fedha za wadhamini wao wote.

Kikosi hicho kwa sasa kinaendelea na maandalizi yake kule Avic Town, Kigamboni wakiwa wanajiandaa na msimu mpya wa ligi.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Abbas Tarimba amesema: “Tunajivunia kwa kufanikisha tukio letu muhimu la uzinduzi wa jezi mpya ambazo bila shaka yoyote ndizo jezi bora zaidi kuiwahi kutengenezwa nasi, hii ni sehemu ya maandalizi yetu ya kabla ya msimu.

“Matarajio ni makubwa kwa msimu ujao na kwa namna ninavyoona mipango inayoendelea kuwekwa hususani katika kuboresha nguvu ya uchumi, basi msimu ujao naiona Yanga ikishinda tena mataji yote matatu na kufanya mambo makubwa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleSIMBA WATAMBA;TUNARUDI NA KASI YA KIBERENGE,MSHTUKO SENZO KUNG’OKA YANGA
Next articleTAIFA STARS WANASTAHILI PONGEZI KIDOGO