TAIFA STARS WANASTAHILI PONGEZI KIDOGO

    USHINDI unaleta furaha,ushindi unaleta kicheko ushindi unarejesha lile tabasamu ambalo lilikuwa limejificha kwenye sura ya yule aliyekuwa na makasiriko.

    Unadhani ushindi unaleta hayo tu,hapana kuna mengi ambayo yanaletwa na ushindi ikiwa ni pamoja na furaha na kuhisi kwamba kila kitu unachogusa kinakutii na kile ambacho hauna mamlaka nacho kinakusikiliza kwa umakini.

    Ushindi upi ambao unaweza kutufanya tukawa na furaha hasa kwa Watanzania pale timu yetu inapoweza kushinda na kusonga mbele katika mechi zao?

    Basi kazi yao ya kwanza kusaka ushindi kwa wawakilishi wa Tanzania, Taifa Stars mbele ya CHAN kumeweza kuleta furaha na tabasamu kwa Watanzania.

    Tumeona wengi walikuwa wanaibeza Somalia na kuiweka kwenye kundi jepesi, hakuna kitu kama hicho kwenye ulimwengu wa mpira,kila timu ni ngumu na inafanya vizuri ulingana na mbinu.

    Ushindi wa mwanza wa bao 1-0 na ule wa pili wa mabao 2-1 umeonyesha kwamba kila mchezo ulikuwa na mbinu tofauti na kikubwa kilichokuwa kinawaka kwenye mioyo ya wachezaji ni kupambana.

    Ilikuwa hivyo mwanzo mwisho vijana wamejitoa katika kusaka ushindi na kuweza kupenya kwenye hatua ya awali na sasa wana kete nyingine dhidi ya Uganda.

    Unaambiwa kwamba liishalo ni dogo kuliko lile ambalo linakuja sasa kigongo kinachofuata ni moto wa kuotea mbali hapo mipango inahitajika.

    Hebu tuwapongeze kidogo wachezaji wa Stars kwa kufanya kazi kubwa na nzuri kwa kuwa wamerejesha ile furaha kwa Watanzania.

    Unaweze kujiuliza kwa nini ninasema tuwapongeze kidogo kisha tuendelee kuwaambia kwamba deni lao bado lipo?

    Jibu ni moja tu kazi ya kwanza wameimaliza hilo wanastahili pongezi kwa kuwa wameshinda lakini wasisahau kwamba wana kazi nyingine mbele kwenye mchezo wao dhidi ya Uganda.

    Wakipokea pongezi nyingi watajisahau na kuendelea kuishi kwenye ulimwengu wa pongezi ambao muda wake tayari umekwisha na kinachotakiwa ni kuendelea kufanya kazi.

    Ushindi kwa mchezo ujao utazidi kuwapa nguvu ya kuendelea kupambana na pongezi pia zitawafuata lakini wasahahu kwamba wanapaswa kuendelea kushindana.

    Yaani maisha ya mpira unashinda kisha unashinda kisha unashinda kisha unashinda tena hapo pongezi zitazidi kuendelea huku kazi ikizidi kuendelea kwani hakuna mwisho wa kushindana mpaka pale utakapofika mwisho.

    Pongezi kubwa kwa mashabiki ambao walikuwa wamejitokeza kwenye mechi zote mbili kuwashangilia vijana wapambanaji waliokuwa wakivuja jasho.

    Pongezi kubwa kwa wachezaji ambao waliweza kulipa kile ambacho mashabiki walikuwa wanastahili kupata kwa wakati huo unadhani ni furaha gani ipo kwenye mioyo ya wachezaji na Watanzania kwa sasa?

    Mashabiki waliojitokeza waliweza kuona kile ambacho walistahili,mpira wa kazi na jasho,burudani na matokeo na mwisho wa yote ushindi kwenye hatua moja kuelekea kwenye hatua nyingine.

    Ipo wazi kwamba hakuna ambaye alitarajia kwamba mngekutana na ushindani ule kwa wapinzani kutokana na namna jasho lilivyokuwa likimwagika mwanzo mwisho.

    Kwa mechi zijazo kazi ipo na maandalizi mazuri yatakuwa ni silaha namba moja kupata ushindi kwa mechi zote kwani mpira ni maandalizi.

    Kila kitu kinawezekana kikubwa ni maandalizi na matumizi ya nafasi ambazo zitapatikana kwenye mchezo wenu ujao na hili kwenu wachezaji.

    Furaha ya mashabiki na Watanzania ipo kwenye matokeo n ahata wachezaji pia wanahitaji matokeo hivyo mipango kwa mechi ijayo ni muhimu na kuongeza umakini zaidi ni kitu cha msingi pia.

    Imeandikwa na Dizo Click.

    Previous articleYANGA YATAMBA KUKOMBA KILA KITU
    Next articleMENEJA MPYA YANGA ATOA SHUKRANI ZAKE KMC