MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais ndani ya Yanga,Suma Mwaitenda ameweka wazi kuwa akipata nafasi ya kuingoza timu hiyo atashirikiana na rais ambaye atachaguliwa.
Julai 9, Yanga inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi ambapo ni kwa upande wa Rais mgombea akiwa ni Injinia Hersi Said na kwa upande wa makamu wa Rais wapo wawili ikiwa ni Arafat Haji pamoja na Suma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni zake makao makuu ya Yanga, Suma amesema kuwa hesabu zake kubwa ni kuweza kuboresha masuala ya mapato pamoja na uwekezaji ndani ya timu hiyo.
“Malengo makubwa ni kuweza kuingoza Klabu ya Yanga kwa kufuata katiba ambao ni muongozo na pia kuweka jitihada za kuongeza wadhamini na kuwalinda hawa ambao wapo ikiwa ni pamoja na SportPesa pamoja na GSM na pia kuweka mfumo mzuri kwa wanachama hata hivyo tumefanikiwa kuongeza mdhamini ambaye ni Azam.
“Nafahamu kuwa Makamu wa Rais ndio msaidizi na nimejipanga kumsapoti na kuendeleza yale ambayo tutafanya ili kuleta mabadiliko na kushirikiana na Rais katika Klabu yetu.
“Nina hitaji kukarabati jengo letu la hapa Jangwani.
lakini pia nitaboresha mpira kwa timu zetu zote hasa ukizingatia kwamba ni kweli kabisa hatujaweza kuchukia mataji timu hizi ndogo lakini pia tunajivunia Yanga baada ya kushinda msimu huu.
“Sehemu ya uchumi na uwekezaji tunaenda kwenye soko la kisasa huko kunahitaji pesa,wanachama na funbase, kusajili na kujenga kikosi imara,naiona Yanga mpya katika miaka 8 ijayo kwa kuwa uzoefu nanao.
“Kuhusu mgombea wa Urais kuweza kuambatana na mgombea makamu wa Rais lakini ambacho ninajua ni kwamba uchaguzi bado haujafanyika na ninajua kwamba hakuna suala la ugombea wenza kama inavyokuwa kwenye siasa,wanachama wa Yanga wanichague nifanye kwa vitendo,” amesema Suma.