Home Sports MTIBWA SUGAR KUCHEZA KAMA FAINALI LEO

MTIBWA SUGAR KUCHEZA KAMA FAINALI LEO

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba utapambana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga kama fainali ili kuweza kupata ushindi.

Mtibwa Sugar ikiwa itapoteza mchezo wa leo inajiweka kwenye nafasi ya kushuka daraja jumlajumla jambo ambalo Mtibwa Sugar hawahalipendi.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 na ina pointi 31 huku Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 71 baada ya kucheza mechi 29.

 Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema:“Mchezo wetu utakuwa ni kama fainali kwa kuwa tukifungwa itakuwa hali mbaya kwetu tunaweza kushuka daraja lakini ambacho tunatakiwa kufanya ni kupata ushindi ama sare.

“Hakuna haja ya kuweza kukata tamaa tunajua kwamba Yanga haijafungwa na sisi tunalitambua hilo tunaweza tukashinda ama tukapata sare yote yanawezekana.

“Tumepata matokeo mabaya mbele ya Namungo tumefungwa kwenye mchezo ule hatujapenda sasa tunakwenda kufunga pazia kwenye mchezo wetu wa kufunga pazia kwenye ligi mbele ya Yanga,tuna Imani ya kufanya vizuri wachezaji wanajua tunachohitaji,” amesema Kifaru.

Previous articleKOCHA WA VIWANGO ATUA SIMBA, ASHAFIKA HATUA YA NUSU FAINALI KOMBE LA AFRIKA
Next articleJESUS ATUA ARSENAL, AFANYA VIPIMO