Home International GABRIEL JESUS KUIBUKIA ARSENAL

GABRIEL JESUS KUIBUKIA ARSENAL

KAMA mambo yakienda sawa, basi wiki ijayo, Arsenal itamtabulisha Gabriel Jesus ambaye wamemnasa kwa pauni 50m akitokea Manchester City.

 Arsenal kumpata straika huyo ni baada ya kuzipiku Tottenham na Chelsea ambazo nazo zilionekana kumuhitaji.

 Inatajwa kwamba, tayari Arsenal imekamilisha dili hilo na vimesalia vitu vichache tu kumaliza kila kitu na wakati wowote atafanyiwa vipimo vya afya.

 Jesus aliweka wazi malengo yake ya kuondoka ndani ya kikosi hicho hasa baada ya ujio wa Erling Haaland kikosini hapo.

 Straika huyo atakuwa ni mchezaji wa nne kutua ndani ya Arsenal kuelekea msimu ujao baada ya kipa Matt Turner, Marquinhos na Fabio Vieira.

 Jesus atakuwa chaguo la kwanza kwa upande wa mastraika kikosini hapo baada ya kuondoka kwa Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette.

Previous articleSTAA HUYU KUTOKA LEEDS UNITED MALI YA MAN CITY
Next articleWINGA WA CHELSEA ZIYECH KUUZWA