WAKATI MWINGINE KUPIGA HESABU KIMATAIFA

    WAKATI mwingine tena wa kukamilisha hesabu kwenye mipango ya kimataifa hasa kwa timu ambazo zinakibarua cha kufanya hivyo kimataifa.

    Haikuwa kazi ngumu kwa msimu uliopita kwa timu za Tanzania kuweza kupeta kimataifa kwa kuwa kila timu ilikuwa inakwenda kwa mwendo wake wa kusuasua.

    Azam FC licha ya kuwa imara kwenye miundombinu pamoja na wachezaji wazuri bado kimataifa walishindwa kututuoa kimasomaso Watanzania.

    Kwa upande wa Yanga nao pia walikwama kufika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku wale waliokuwa wanapewa nafasi ya kufanya vizuri kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

    Simba ambao walitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu walifungashiwa virago mapema kwenye Ligi ya Mabingwa na kuangukia Kombe la Shirikisho.

    Kwa yote ambayo wamefanya licha ya kuishia hatua ya robo fainali bado tulishindwa kuwa na wawakilishi kwenye Ligi ya Mabingwa.

    Muda huu ambao upo hasa ligi ikifika ukingoni ni wakati sahihi wa kuweza kuanza kuweka mipango upya kwa ajili ya wakati ujao.

    Tunaamini kwamba timu zote zimejua pale ambapo walikwama hivyo watakuwa kwenye hesabu nzuri kwa msimu ujao kwa kuwa watakuwa na muda wa kufanyia kazi makosa.

    Muhimu kutambua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo mazuri na kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa hilo ni jambo la msingi litakalodumisha tabasamu

    Previous articleMASHINE YA MABAO SIMBA KUPEWA MKONO WA KWA HERI
    Next articleNGUVU IWE KUBWA MAANDALIZI KOMBE LA DUNIA