Home Sports MASHINE YA MABAO SIMBA KUPEWA MKONO WA KWA HERI

MASHINE YA MABAO SIMBA KUPEWA MKONO WA KWA HERI

MEDDIE Kagere mshambuliaji wa mabao ndani ya Simba anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa ambao watapigwa chini ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki ligi.

Simba leo ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa tayari mabosi wa Simba wameanza mpango wa kusaka mbadala wa Kagere ili aweze kuingia moja kwa moja kikosini.

“Kwa sasa Simba inahitaji kuongeza mshambuliaji mwenye kasi na spidi hivyo mpango namba moja ni kuweza kumpa mkono wa shukrani Kagere,” ilieleza taarifa hiyo.

Msimu huu Kagere ambaye ametwaa tuzo ya ufungaji bora mara mbili ametupia mabao 7 ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kaimu Kocha Seleman Matola.

Previous articleYANGA RAHA,KIUNGO MALI AUBALI KUTUA SIMBA
Next articleWAKATI MWINGINE KUPIGA HESABU KIMATAIFA