Home Sports SIMBA YANYOOSHWA KIDUDE KIMOJA NA PRISONS

SIMBA YANYOOSHWA KIDUDE KIMOJA NA PRISONS

WAKIWA Uwanja wa Sokoine, Mbeya leo Simba wamechezeshwa pira gwaride kwa kunyooshwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Ni Benjamin Asukile ambaye alipachika bao la ushindi kwa Prisons ilikuwa dk ya 59 na kuwafanya Simba kuambulia maumivu ugenini.

Tanzania Prisons wameweza kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo walifungwa bao 1-0 na kuwafanya waache pointi tatu mazima.

Mchezo wa leo ni wa nne kwa Seleman Matola ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa Simba kukaa kwenye benchi baada ya kuchukua mikoba ya Pablo Franco ambaye alifutwa kazi.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Matola kupoteza leo wa kuwa kwenye mechi tatu aliweza kushuhudia vijana wake wakisepa na pointi tatu jumlajumla.

Jitihada za Peter Banda kiungo wa Simba akishirikiana na Meddie Kagere,Kibu Dennis kupenya ngome ya Tanzania Prisons ziligonga mwamba.

Previous articleUWANJA WA SOKOINE:PRISONS 0-0 SIMBA
Next articleVIDEO: ONA MAYELE AVAMIA SHOW/VIBE LAKE BALAA MWANZO MWISHO