Home Sports MAN UNITED KUITIBULIA ARSENAL KWA RAPHINHA

MAN UNITED KUITIBULIA ARSENAL KWA RAPHINHA

UWEZO mkubwa aliouonyesha staa wa Leeds United, Raphinha kwa kuisaidia timu hiyo kusalia ndani ya Ligi Kuu England imezivutia klabu za Tottenham, Liverpool na Manchester United ambao sasa wameingia katika mbio hizo dhidi ya Arsenal ambayo tayari imetenga dau la pauni milioni 50.

Mbrazil huyo alikuwa kinara wa mabao ndani ya kikosi cha Leeds msimu uliopita ambapo mabao yake 11 yalionekana kuwa muhimu. Arsenal wako tayari kutoa dau la pauni milioni 50 huku Mikel Arteta akitafuta kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, wapinzani wao wa London kaskazini Tottenham nao wana nia.

Vigogo wa Uhispania Barcelona pia wana nia ya kumsajili staa huyo huku ikielezwa kuwa wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu na ushawishi wa nyota kama, Luis Suarez na Philippe Coutinho ukiongeza uwezekano huo.

Nyota wa Man United, Bruno Fernandes amewahi kucheza na Raphinha walipokuwa Sporting Lisbon, ambapo Fernandes akimzungumzia Raphinha alinukuliwa akisema: “Raphinha, ninamkumbuka Raphinha. Ni mchezaji ambaye nilikuwa na muunganiko mzuri tukiwa Lisbon, pia ninamkumbuka kwa ucheshi wake kwenye chumba cha kubadilishia nguo na ni mtu anayewajibika na anayefanya kazi kwa bidii.”

Previous articleMERIDIANBET WAAHIDI KUENDELEA KUSAPOTI SOKA LA WANAWAKE!
Next articleARSENAL YAKOMAA NA JESUS MCHEZAJI WA MAN CITY