Home Sports ARSENAL YAKOMAA NA JESUS MCHEZAJI WA MAN CITY

ARSENAL YAKOMAA NA JESUS MCHEZAJI WA MAN CITY

MAWAKALA wa Straika wa Manchester City, Gabriel Jesus wamesafiri mpaka nchini Uingereza kwa ajili ya kuhakikisha wanakamilisha dili la straika huyo ambaye anatajwa kutua ndani ya Arsenal kutokea Manchester City.

 

Mabingwa hao wa Premier wanataka pauni milioni 50 kwa Jesus, huku wakitarajia kurejesha fedha hiyo ili kufidia matumizi yao kwa, Kalvin Phillips wa Leeds United na Marc Cucurella wa Brighton.

 

Jesus amekaa miaka mitano iliyopita akiwa na City, lakini anataka kuondoka msimu huu wa joto baada ya kuchagua kutoongeza mkataba wake unaotarajiwa kumalizika mwakani kutokana na kuhofia nafasi yake kikosini baada ya usajili wa Erling Haaland.

 

City walikataa ofa ya awali ya Arsenal ya pauni milioni 35 pamoja na nyongeza, na inaelezwa kuwa Arsenal wanajipanga kuwasilisha ofa nyingine.

 

Wakati huohuo Arsenal wamekuwa na majadiliano chanya juu ya uhamisho wa winga wa Leeds United Raphinha ambaye alimaliza msimu uliopita kama mfungaji bora wa Leeds katika michuano yote akiwa na mabao 11.

 

Previous articleMAN UNITED KUITIBULIA ARSENAL KWA RAPHINHA
Next articleBUGATTI LA RONALDO LAPATA AJALI