Home Uncategorized DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA JULAI 1, 2022 …KUFUNGWA AGOSTI 31

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA JULAI 1, 2022 …KUFUNGWA AGOSTI 31

Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 litafunguliwa Julai 1, 2022 na kufungwa Agosti 31, 2022.

Katika kipindi hicho Klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.

Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana a changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.

Aidha Dirisha Dogo lenyewe litafunguliwa Desemba 16, 2022 na kufungwa Januari 15, 2023.

Previous articleYANGA YAFUNGUKIA USAJILI WA AZIZ KI
Next articleYANGA MAFIA… STRAIKA WA MABAO AWAZIMIA SIMU SIMBA