Home Sports KOCHA MPYA SIMBA ATUA NA MAJEMBE MATATU YA KAZI

KOCHA MPYA SIMBA ATUA NA MAJEMBE MATATU YA KAZI

UNAAMBIWA mchakato wa kupitia wasifu wa kumpata Kocha Mkuu wa Simba atakayerithi mikoba ya Pablo Franco, umekamilika na kwamba, kocha ajaye muda si mrefu atatangazwa kikosini hapo.

Hadi kufikia jana, kulikuwa na makocha wawili ambao walikuwa wakiangaliwa kwa mara ya mwisho ili mmoja kupitishwa akiwemo kocha wa zamani wa RS Berkane ya Morocco raia nchi hiyo, Tarik Sektioui. Mwingine ni Jozef Vukušič raia wa Slovakia.

Wakati makocha hayo wakitajwa, imeelezwa kwamba, kocha ambaye anatarajiwa kupitishwa, ameomba kuja na majembe matatu ya kazi akiwemo kocha wa viungo na wachezaji wawili.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, zinasema kwamba, Sektioui ana nafasi kubwa ya kupewa mikoba hiyo.

Kocha huyo Oktoba 25, 2021, alikiongoza kikosi cha RS Berkane kutwaa Kombe la Shirikisho la CAF kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeweka wazi kwamba, baada ya uongozi kuchakata na kufanya mahojiano na makocha waliosalia kwenye ile orodha ya waliokuwa wakiwahitaji, Sektioui ameonekana kuwa na nafasi kubwa.

“Tayari tumeshapata kocha mkuu na kwamba taratibu zote za usajili unaoendelea kwetu, yeye ndiye ameshauri, ambapo miongoni mwa wachezaji waliokwishazungumza nasi, wawili atakuja nao mwenyewe pamoja na kocha wa viungo.

“Atakuja na kiungo mkabaji pamoja na straika mkali wa mabao, pia ametuelekeza kumsajili beki wa kati na winga ambaye yeye majina anayo,” kilisema chanzo hicho.

Kocha huyo Machi 7, 2021, alijiuzulu kuitumikia RS Berkane na nafasi yake ikachukuliwa na Kocha Juan Pedro Benali, raia wa Hispania, alipoondoka akateuliwa Florent Ibenge ambaye yupo hadi sasa.

Timu ya mwisho kufundisha Sektioui ni Emirates ya UAE, ambayo aliitumikia kwa msimu wa 2021, 22.

Previous articleUSAJILI WA KIUNGO MNIGERIA SIMBA KAMA MUVI
Next articleSIMBA NOMA YATUMIA UJANJA KUMNASA KIUNGO FUNDI