Home Sports SOPU APIGIWA HESABU NA VIGOGO VITATU

SOPU APIGIWA HESABU NA VIGOGO VITATU

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye hesabu za kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Coastal Union,Abdul Suleiman,’Sopu’.

Sopu amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo anaongoza kwa utupiaji wa mabao akiwa nayo 7 kwenye ligi.

Ikumbukwe kwamba kiungo huyo amecheza Simba kisha akaibukia Ndanda kwa mkopo na akaibuka ndani ya Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda.

Katikati ya mpango wa Simba kuiwania saini ya kiungo huyo inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga wakampigia simu Sopu na kumuulizia suala la mkataba wake ili wajue kama wanaweza kufanya jambo.

Ngoma ikiwa inachezwa pale Uwanja wa Mkapa na Yanga, unaambiwa Azam nao walikuwa wakimfuatilia ili kuweza kuinasa saini yake.

Hivyo ni vigogo watatu wanawania saini yake ikiwa ni Yanga, Azam na Simba.

Kwa upande wa Coastal Union mtu wa ndani amesema kuwa hakuna ofa ambayo wamepata kwa ajili ya mchezaji huyo.

Tags 

Previous articleSIMBA KAMILI KUIVAA KMC
Next articleTEAM KIBA WAWANYOOSHA TEAM SAMATTA