Home Sports AZIZ KI ATAJWA KUMALIZANA NA MABOSI MSIMBAZI

AZIZ KI ATAJWA KUMALIZANA NA MABOSI MSIMBAZI

KIUNGO mshambuliaji wa Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast, Stephane Aziz Ki anatajwa kumalizana na mabosi wa Simba kwa dili la miaka miwili.

Nyota huyo anatajwa kuingia kwenye rada za watani wa jadi wa Simba ambao ni Yanga waliokuwa kwenye mazungumzo naye.

Dili ambalo Yanga walitajwa kumpa ilikuwa ni miaka mitatu na kilichokuwa kimebaki ni kuweza kusaini mkataba wa kuweza kujiunga na timu hiyo.

Hivi karibuni Injinia Hers Said aliweka wazi kuwa kwa namna ambavyo timu hiyo imekuwa ikifanya vizuri ni wachezaji wanahitaji kucheza ndani ya timu hiyo.

“Kwa ambapo tumefikia kwa sasa ni wachezaji wanahitaji kucheza hapa kwani timu inafanya vizuri na matokeo yanaonekana.

“Kuhusu usajili tutasajili wachezaji wazuri zaidi ambao watakuwa nasi kwenye mashindano ya kimataifa,”.

Previous articleKIUNGO WA SIMBA AREJEA
Next articleMSIMU UNAFIKA UKINGONI SASA HESABU MUHIMU