Home Sports MSIMU UNAFIKA UKINGONI SASA HESABU MUHIMU

MSIMU UNAFIKA UKINGONI SASA HESABU MUHIMU

WAKATI uliobaki kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara ni mdogo hasa ukizingatia kwamba mechi zilizobaki hazizidi 7 kwa timu zinazoshiriki ligi hivyo ni muda wa kukamilisha hesabu.

Matokeo ambayo yanapatikana leo ni maandalizi ya jana hivyo kwa sasa ni muda wa kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kesho.

Tunaona kwamba wapo wachezaji ambao kwa sasa kandarasi zao zinakaribia kufika ukingoni na wapo wale ambao tayari timu zimeweka wazi kwamba hawatakuwa nao kwa ajili ya msimu ujao.

Muhimu ambacho kinapaswa kuangaliwa kwa sasa ni kila mmoja kufanya mambo kwa umakini bila kukurupuka hasa kwenye wakati huu wa kukamilisha mzunguko wa pili.

Jambo la msingi ni kuona kila kitu kinakwenda kwa mipango ambayo imepangwa hasa ukizingatia ni mwisho wa msimu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Kwenye usajili hapo itapendeza kila timu ikapitia ripoti ya benchi la ufundi na kuacha ifanye kazi hasa kwa kuboresha yale maeneo ambayo yanahitajika na maeneo ambayo yalikuwa hayajawa bora.

Msimu ujao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hasa ukizingatia kwamba kila mmoja ana kazi ya kutimiza yale ambayo wanahitaji kuyafanya.

Muda ni huu kufanya maandalizi mazuri kwa wakati ujao msimu ambao unatarajiwa kuwa mgumu zaidi na wenye ushindani mkubwa zaidi.

Previous articleAZIZ KI ATAJWA KUMALIZANA NA MABOSI MSIMBAZI
Next articleKMC HESABU ZAO ZA MZUNGUKO WA PILI ACHA KABISA