STAA wa Tottenham Harry Kane alikuwa ni mwiba mkali mbele ya Arsenal baada ya kuwatungua mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Alianza kufunga dk ya 22 kwa mkwaju wa penalti kisha bao la pili alipachika dk ya 37 na msumari wa tatu ulipachikwa na nyota Son ilikuwa dk ya 47.
Mpaka dk 90 zinakamilika Uwanja wa Tottenham ulikuwa unasoma Spurs 3-0 Arsenal.
Kwenye msimamo Tottenham ipo nafasi ya 5 na pointi 65 huku Arsenal ikiwa nafasi ya 4 na pointi 66.