MNYAMA RONALDO AFANYA YAKE

MBELE ya mashabiki 73,564 waliojitokeza Uwanja wa Old Trafford, Cristiano Ronaldo aliweza kufunga bao ambalo liliacha pointi moja kwa Manchester United.

Ilikuwa dk ya 62 alisawazisha bao lililofungwa na Marcos Alonso wa Chelsea aliyefunga bao hilo dk ya 60.

Hivyo wababe hao walikamilisha dakika 90 ubao ukisoma Manchester United 1-1 Chelsea.

Ni Reece James wa Chelsea amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.