LIVERPOOL imeichapa Manchester United mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield.
Ni mabao mawili.ya Mohamed Salah huku moja lile la ufunguzi likifungwa na Luis na moja lilifunvwa na Sadio Mane.
Thiago amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo kwa kuwa alikuwa ni mtengeneza mipango ya pasi ndani ya Anfield.
Liverpool ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 76 huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na pointi 74 ila ina mchezo mmoja mkononi.