CHELSEA SAFARI IMEWAKUTA,BENZEMA TATIZO

REAL Madrid safari ya nusu fainali ya Champions League imejibu baada ya ushindi wa jumla ya mabao 5-4 dhidi ya Chelsea.

Ni Karim Benzema ambaye alikuwa ni mwiba kwa Chelsea baada ya kupachika bao la ushindi kwa Real Madrid katika muda wa nyongeza.

Ilikuwa ni Uwanja wa Santiago Bernabeu mbele ya mashabiki 59,839 ubao ulisoma Real Madrid 2-3 Chelsea.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dk 15, Antonio Rudiger dk 51 na Timo Werner dk 75.

Bao la kwanza kwa Real Madrid lilifungwa na Rodrgo dk 80 ambaye aliweza kuongeza nguvu kwa Real Madrid kusaka ushindi.

Thomas Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa alikasirishwa na kitendo cha kumuona mwamuzi anacheka Kocha Mkuu wa Real Madrid.

“Sijapenda kwa kweli kumuona mwamuzi akiwa na muda mzuri na Carlo, (Ancelotti) muda ambao nataka kumwambia asante alikuwa anacheka na kocha wa timu pinzani,”.