Home Sports MAYELE ALIWEKWA MTU KATI UWANJA WA MKAPA NA NYOSSO

MAYELE ALIWEKWA MTU KATI UWANJA WA MKAPA NA NYOSSO

FISTON Mayele mshambuliaji wa Yanga aliwekwa mtu kati juzi mbele ya Geita Gold baada ya kukabidhiwa kwenye mikono salama ya Kelvin Yondan na Juma Nyosso ambao walikula naye sahani moja.

Mzee huyo wa kutetema aliyeyusha dk 90 mazima bila kutetema huku kila hatua ambayo anakwenda nyuma alikuwa yupo Nyosso ama Yondani kwa ajili ya kwenda naye sawa.

Kutokana na kubanwa kwa nyota huyo ambaye ni kinara wa utupiaji ndani ya ligi akiwa ametupia mabao 11 juzi hakupiga shuti hata moja ambalo lililenga lango.

Alitoa jumla ya pasi 25 na ni 17  alitoa kwa mguu wa kulia ule wa kushoto pasi 3 na alipiga vichwa mipira mara tatu huku kwa kifua akitoa pasi 2.

Kutokana na kubwana huko nyota huyo alichezewa faulo moja na yeye alicheza pia faulo moja katika mchezo huo wa hatua ya robo fainali.

Licha ya kuwekwa mtu kati, Yanga imetinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 7-6 na katika wapigaji wa penalti moja ilifungwa na Mayele mwenyewe.

Previous articleAIR MANULA KIMATAIFA MWENDO WAKE
Next articleVIDEO:SIMBA YATUPA DONGO KWA WATANI KIMTINDO,YAWAITA MASHABIKI