KAZI YA JOB ACHA

DICKSON Job, beki wa kati wa kikosi cha Yanga juzi alipiga kazi kwelikweli kwa kushirikiana na wahezaji wenzake ikiwa ni pamoja na Bakari Mwamnyeto,Yanick Bangala mbele ya Geita Gold.

Beki huyo wa kati wakati Yanga ikitinga hatua ya nusu fainali aliyeyusha dk 90 na alikuwa ni mtengeneza mipango eneo la kati kwa kuwa pasi zilianzia kwake Uwanja wa Mkapa.

Alipiga jumla ya pasi 52 huku akitumia mguu ule wa kulia kwa asilimia kubwa ambapo alipiga pasi 46 ule wa kushoto alipiga pasi 3.

Uwezo wake pia ulikuwa kwenye mwendo akiwa na mpira ambapo alikokota mara 22 ile mipira ya juu alikwenda nayo pia hewani na alipiga vichwa mara 3.

Pia Job alipiga shuti moja ambalo lililenga lango ilikuwa dk ya kwanza na katika pasi hizo 52 ambazo alipiga asilimia 99 zilifika sehemu sahihi huku moja aliyopiga dk ya 71 haikufika mahali pake alipokuwa amekusudia ifike.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 7-6 dhidi ya Geita Gold pia nyota huyo aliweza kupiga penalti ambayo ilijaa wavuni.