ERIC ten HAG KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

ERIC ten Hag anatajwa kuwa kwenye mpango wa kujiunga na Klabu ya Manchester United kwa ajili ya kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Kwa sasa Hag yupo ndani ya kikosi cha Ajax akiwa ni kocha katika timu hiyo.

Inaelezwa kuwa Manchester United wanahiraji kupata huduma yake ili aweze kuwa ndani ya Old Trafford kwa msimu ujao.

Kwa sasa anatajwa kuwa katika mazungumzo na United ili kuona namna gani anaweza kwenda kuinoa timu hiyo.

Kwa sasa United inanolewa na Kocha Mkuu, Ralf Rangnick ambaye amekuwa kwenye mwendo wa kusuasua na timu hiyo na alipoteza mchezo uliopita mbele ya Everton kwa kufungwa bao 1-0 Aprili 9,2022.