SIMBA QUEENS WANATAKA ALAMA TATU

MENEJA wa Simba Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), Selemani Makanya, amesema wachezaji wamejiandaa vema kuikabili Ruvuma Queens katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makanya alisema: “Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huu, hakuna majeruhi, wachezaji wote wapo vizuri.

 

“Wapinzani wetu raundi ya kwanza tuliwafunga mabao 15, hii ni raundi ya pili, inawezekana wamekaa chini wakajiuliza wapi waliosea, kikubwa hatuwezi kuwadharau, tutaingia kwa tahadhari kubwa nia ni kupata alama tatu.”