SALAH AFUNGUKIA ISHU YA MKATABA WAKE

MOHAMED Salah, mshambuliaji wa Liverpool ameweka wazi kuwa ishu ya mkataba wake kwa sasa ndani ya kikosi hicho hawezi kusema ndiyo ama hapana.

Salah mkataba wake ndani ya Liverpool unatarajiwa kumalizika Juni 2023.Mpaka sasa haijaweza kuwekwa wazi kuhusu makualiano yake na timu hiyo.

Salah alipoulizwa kuhusu mkataba wake amesema:”Niwe mkweli,kuna vitu vingi watu hawavijui sitaki kuwa mbinafsi na kuzungumza mambo yangu kwa sasa.

“Natakiwa kuzungumza kuhusu timu na kuangalia yaliyopo mbele yetu hicho ndiyo kitu muhimu kwa sasa.

“Kuhusu mkataba siwezi kusema hapana au ndiyo,hili nimeshalizungumza mara nyingi na siwezi kuliongelea tena,”.