ZIMETINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,KUKUTANA NA SIMBA

UKIIWEKA kando Simba kutoka Tanzania pamoja na RS Berkane kutoka Morocco ambazo hizi zipo kundi D pia zipo nyingine ambazo ziliweza kutinga hatua ya roo fainali.

Timu hizo ni pamoja na Al Ahly Tripoli ya Libya na Pyramids ya Misri hizi zilikuwa kundi A.

Orlando Pirates ya Afrika Kusini na A Ittihad ya Libya kutoka kundi B.

TP Mazembe ya DR Congo na Al Masry ya Misri kutoka kundi C.

Kesho Jumanne inatarajiwa kuchezwa droo ya mechi za robo fainali na Simba inaweza kukutana na Al Ahly Tripoli, Orlando Pirates au TP Mazembe ambazo zimemaliza vinara katika makundi yao.