MANCHESTER UNITED WAAMBIWA NGUMU KUWA TOP 4

GARY Neville, mchambuzi wa masuala ya michezo anaamini kwamba mbio za timu yake hiyo ya zamani kutinga top 4 ni ngumu baada ya kutoshana nguvu na Leicester City,Uwanja wa Old Trafford.

Bao la Kelechi Iheanacho dk 63 kwa Leicester City kisha United waliweka usawa kupitia kwa Fred dk ya  66.

Kwenye msimamo United ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 51 sawa na Wast Ham United iliyo nafasi ya 6 na imecheza mechi 31.

Nevile amesema:”Nadhani mapumziko ya timu za kimataifa yangewasaidia lakini mambo yamekuwa tofauti kwa kuwa sasa mambo yanakuwa magumu kwao kuweza kumaliza ndani ya Top 4,”.