BANDA APEWA MILIONI SIMBA

PETER Banda kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ni jambo kubwa kwake kuweza kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi.

Banda ni Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) na amepewa zawadi yake baada ya kuwashinda Shomari Kapombe na Pape Sakho ambao aliingia nao fainali.

Banda amepewa zawadi ya shilingi milioni mbili baada ya kuweza kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kutokana na kile ambacho mchezaji anakifanya ndani ya kikosi hicho.

Kiungo huyo amesema:”Ninafurahi kuweza kupewa zawadi hii na ni furaha kubwa kwani inanifaya niweze kuongeza juhudi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza na kazi bado ipo.

“Ambacho ninaweza kusema shukrani kwa mashabiki pamoja na wachezaji wenzangu ambao tumekuwa tunashirikiana kwenye kazi,”amesema.