Home International AUBA MWENDO WA REKODI TU

AUBA MWENDO WA REKODI TU

STAA wa Klabu ya Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang amezidi kuwa moto ndani ya maisha yake mapya ambayo ameyeanza kuishi kwa sasa.

Jumapili nyota huyo alikuwa mchezaji aliyefanya vizuri kwenye El Clasico wakati Barcelona iliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Real Madrid wakiwa ugenini.

Alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja jambo ambalo ni kubwa kwake tangu alipojiunga bure na timu hiyo inayoshiriki La Liga akitokea Arsenal ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Kwenye mchezo huo staa huyo alitumia dakika 71 na tangu ametua hapo Januari mwaka huu amekuwa ni moto wa kuotea mbali.

Pia ana rekodi ya kuweza kufunga hat trick ndani ya La Liga ilikuwa mbele ya Valencia na ni dakika 444 ametumia kwenye La Liga.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleSERENGETI GIRLS WAREJEA BONGO NA USHINDI