BARCELONA YAICHAPA MABAO 4-0 REAL MADRID

WAKIWA Uwanja wa Santiago Bernabeu wameshuhudia ubao ukisoma Real Madrid 0-4 Barcelona.

Pierre Aubameyang alitupua 2 dk 29 na 51,Ronald Araujo dk 38 na Ferran Torres dk 47.

Mchezo huo wa El Clasico umiliki ulikuwa ni mali ya Barcelona ambao walikuwa na asilimia 60 huku Real Madrid wao ikiwa ni 40.

Ushindi huo unaifanya Barcelona kufikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya 3 na vinara bado ni Real Madrid na pointi zao no 66 kibindoni.