Home Uncategorized HESABU ZA SIMBA KUTINGA FAINALI KIMATAIFA IPO HIVI

HESABU ZA SIMBA KUTINGA FAINALI KIMATAIFA IPO HIVI

HUKU wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo wao wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kama wakifanikiwa kufuzu robo fainali ya michuano hiyo, basi watakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufika fainali.

Simba inaongoza Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi saba walizokusanya katika michezo minne, wakifuatiwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast wenye pointi sita sawa na RS Berkane kutoka Morocco, huku US Gendarmerie ya Niger wakibuluza mkia na pointi zao nne.

Jumapili hii Simba inatarajiwa kushuka Stade de l’Amitie nchini Benin, kwa ajili ya mchezo wao wa tano dhidi ya ASEC Mimosas.

Akizungumza na Spoti Xtra, Tshabalala alisema: “Tunashukuru kwa nafasi ambayo tupo kwenye msimamo, tumesaliwa na michezo miwili muhimu ambapo tunahitaji kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ili kufuzu hatua ya robo fainali.

“Tunaamini katika ubora ambao kikosi chetu kinaendelea kuuonyesha katika michuano hii, ni wazi kama tutafanikiwa kufuzu robo fainali, basi uzoefu tulioupata msimu uliopita kwenye hatua hiyo utatusaidia kufika fainali.”

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleLEEDS UNITED WAPINDUA MEZA MBELE YA WOLVES