YANGA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA KMC
MSAKO wa pointi tatu umekamilika na ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 2-0 KMC. Mabao ya Andrew Vincent aliyejifunga dk 39 na Djuma Shaban dk 51. KMC walikosa utulivu hali iliyofanya wakose nafasi walizotengeneza na ni kadi 5 za njano wameonyeshwa. Yanga inafikisha pointi 48. KMC inakwama kupata pointi mbele ya Yanga msimu huu…